078 - An-Nabaa

 

 

 

  النَّبَاء

An-Nabaa: 078

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ ﴿١﴾

1. Kuhusu nini wanaulizana?

 

 

عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ ﴿٢﴾

2. Kuhusu habari adhimu.

 

 

الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ﴿٣﴾

3. Ambayo wao wanakhitilafiana kwayo.

 

 

كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. Laa hasha! Hivi karibuni watajua.

 

 

ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٥﴾

5. Kisha laa hasha! Hivi karibuni watajua.

 

 

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا ﴿٦﴾

6. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa tandiko?

 

 

وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا ﴿٧﴾

7. Na milima kuwa kama vigingi?

 

 

 

وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا ﴿٨﴾

8. Na Tukakuumbeni kwa jozi; wanaume na wanawake!

 

 

وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا ﴿٩﴾

9. Na Tukafanya usingizi wenu mnono, kuwa mapumziko (kama kufa)!

 

 

وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ﴿١٠﴾

10. Na Tukafanya usiku kuwa kama libasi la kufunika!

 

 

وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ﴿١١﴾

11. Na Tukafanya mchana kuwa ni wa kutafutia maisha!

 

 

وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا ﴿١٢﴾

12. Na Tukajenga juu yenu (mbingu) saba imara!

 

 

وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ﴿١٣﴾

13. Na Tukafanya siraji yenye mwanga mkali iwakayo kwa nguvu!

 

 

 

وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا ﴿١٤﴾

14. Na Tukateremsha kutoka mawingu yaliyokurubia kunyesha, maji yenye kutiririka kwa kasi kubwa!

 

 

لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا ﴿١٥﴾

15. Ili Tutoe kwayo nafaka na mimea. 

 

 

وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا ﴿١٦﴾

16. Na mabustani yanayosongomana na kuota teletele.

 

 

إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا ﴿١٧﴾

17. Hakika siku ya hukumu na kutenganisha ina wakati maalumu.

 

 

 

يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا ﴿١٨﴾

18. Siku litakapopulizwa baragumu, mtakuja makundi makundi.

 

 

وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا ﴿١٩﴾

19. Na mbingu zitafunguliwa, zitakuwa milango ya njia.

 

 

وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ﴿٢٠﴾

20. Na milima itaendeshwa na itakuwa kama sarabi.

 

 

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾

21. Hakika Jahannam itakuwa yenye kuvizia.

 

 

لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾

22. Kwa walioruka mipaka wakaasi, ndio mahali pao pa kurejea.

 

 

لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾

23. Watabakia humo dahari nyingi.

 

 

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾

24. Hawatoonja humo cha baridi wala kinywaji.

 

 

إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾

25. Isipokuwa maji yachemkayo mno na usaha.

 

 

جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾

26. Jazaa inayowafikiana kabisa.

 

 

 

إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾

27. Hakika wao walikuwa hawataraji kuhesabiwa.

 

 

وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾

28. Na walikadhibisha Aayaat na Ishara Zetu kwa njia zote!

 

 

 

وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾

29. Na kila kitu Tumekitia hesabuni barabara kwa kuandika.

 

 

فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴿٣٠﴾

30. Basi onjeni, kwani Hatutokuzidishieni isipokuwa adhabu.

 

 

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾

31. Hakika wenye taqwa watapata mafanikio.

 

 

حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾

32. Mabustani na mizabibu.

 

 

وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾

33. Na wanawake wenye matiti ya kisichana, wa hirimu moja na waume zao.

 

 

وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤﴾

34. Na kombe lililojaa pomoni mvinyo.

 

 

لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ﴿٣٥﴾

35. Hawatosikia humo upuuzi wala kukadhibisha ukadhibisho.

 

 

 

جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ﴿٣٦﴾

36. Jazaa kutoka kwa Rabb wako, tunukio la kutosheleza.

 

 

رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَـٰنِۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ﴿٣٧﴾

37. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, Ar-Rahmaan. Hawatoweza kumsemesha.

 

 

يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ﴿٣٨﴾

38. Siku atakayosimama Ruwh (Jibriyl) na Malaika safusafu. Hawatozungumza isipokuwa yule ambaye Ar-Rahmaan Amempa idhini na atasema yaliyo sahihi.

 

 

ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا ﴿٣٩﴾

39. Hiyo ni Siku ya haki. Basi atakaye, na ashike marudio kuelekea kwa Rabb wake.

 

 

 

إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا ﴿٤٠﴾

40. Hakika Sisi Tumekuonyeni adhabu ya karibu. Siku mtu atakapotazama yale iliyokadimisha mikono yake, na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa mchanga.

 

 

 

 

 

 

Share