083 - Al-Mutwaffifiyn

 

 

 

  الْمُطَفِّفِين

Al-Mutwaffifiyn: 083

 

 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ ﴿١﴾

1. Ole kwa wanaopunja.

 

 

الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ ﴿٢﴾

2. Ambao wanapopokea kipimo kwa watu wanataka wapimiwe kamilifu.

 

 

وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ﴿٣﴾

3. Na wanapowapimia (watu) kwa kipimo au wanawapimia kwa mizani wanapunja.

 

 

أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾

4. Je, hawadhanii kwamba wao watafufuliwa?

 

 

لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾

5. Kwenye Siku iliyo kuu kabisa.

 

 

يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾

6. Siku watakayosimama watu kwa Rabb wa walimwengu.

 

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ ﴿٧﴾

7. Laa hasha! Hakika kitabu cha watendaji dhambi bila shaka kimo katika Sijjiyn.

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ ﴿٨﴾

8. Na lipi litakalokujulisha nini hiyo Sijjiyn?

 

 

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٩﴾

9.  Ni Kitabu kimeandikwa na kurekodiwa barabara (matendo). 

 

 

وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٠﴾

10. Ole Siku hiyo kwa wakadhibishaji.

 

 

الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿١١﴾

11. Ambao wanaikadhibisha Siku ya malipo.

 

 

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ ﴿١٢﴾

12. Na haikadhibishi isipokuwa kila mwenye kutaadi, mtendaji dhambi.

 

 

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾

13. Anaposomewa Aayaat Zetu, husema: Hekaya za watu wa kale.

 

 

كَلَّاۖ بَلْۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾

14. Laa hasha! Bali imefanya kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ ﴿١٥﴾

15. Laa hasha! Hakika wao Siku hiyo bila shaka watawekewa kizuizi wasimuone Rabb wao.

 

 

ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ ﴿١٦﴾

16. Kisha hakika wao bila shaka wataingizwa na waungue katika moto uwakao vikali mno.

 

 

 

ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿١٧﴾

17. Kisha itasemwa: Haya ndio yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.

 

 

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ﴿١٨﴾

18. Laa hasha! Hakika kitabu cha Waumini watendao wema kwa wingi bila shaka kiko katika ‘Illiyyiyn.

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ ﴿١٩﴾

19. Na lipi litakalokujulisha nini hiyo ‘Illiyyiyn?

 

 

كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٢٠﴾

20. Ni Kitabu kimeandikwa na kurekodiwa barabara (amali).

 

 

يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢١﴾

21. Watakishuhudia waliokurubishwa (kwa Allaah).

 

 

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿٢٢﴾

22. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi  bila shaka watakuwa kwenye neema (taanasa, furaha n.k).

 

 

 

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٢٣﴾

23. Kwenye makochi ya fakhari wakitazama.

 

 

تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾

24. Utatambua nyuso zao kwa nuru ya neema (taanasa, furaha)

 

 

 

يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ ﴿٢٥﴾

25. Watanyweshwa kinywaji safi na bora kabisa cha mvinyo kilichozibwa.

 

 

خِتَامُهُ مِسْكٌۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ ﴿٢٦﴾

26. Mwisho wake ni miski. Na katika hayo basi washindane wenye kushindana.

 

 

وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ ﴿٢٧﴾

27. Na mchanganyiko wake ni kutokana na Tasniym.

 

 

عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢٨﴾

28. Ni chemchemu watakayokunywa humo watakaokurubishwa (kwa Allaah).

 

 

إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ ﴿٢٩﴾

29. Hakika wale waliofanya uhalifu walikuwa (duniani) wakiwacheka wale walioamini.

 

 

وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ ﴿٣٠﴾

30. Na wanapowapitia wanakonyezana.

 

 

وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ ﴿٣١﴾

31. Na wanaporudi kwa ahli zao, hurudi wenye kufurahika kwa dhihaka.

 

 

وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ ﴿٣٢﴾

32. Na wanapowaona, husema: Hakika hawa bila shaka ndio waliopotea.

 

 

وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ ﴿٣٣﴾

33. Na wao hawakutumwa kuwa ni walinzi juu yao.

 

 

 

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ ﴿٣٤﴾

34. Basi leo wale walioamini watawacheka makafiri.

 

 

عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٣٥﴾

35. Kwenye makochi ya fakhari wakitazama.

 

 

هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾

36. Je, basi makafiri wamelipwa yale waliyokuwa wakiyafanya? 

 

 

 

Share