104 - Al-Humazah

 

 

 

  الْهُمَزَة

Al-Humazah: 104

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾

1. Ole kwa kila mwenye kukebehi na kukashifu watu kwa ishara na vitendo, na kwa kila mwenye kufedhehesha kwa ulimi.

 

 

الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ ﴿٢﴾

2. Ambaye amekusanya mali na kuyahesabu.

 

 

يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ ﴿٣﴾

3. Anadhani kwamba mali yake itamdumisha milele.

 

 

كَلَّاۖ لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴿٤﴾

4. Laa hasha! Atavurumishwa katika Al-Hutwamah (moto mkali unaonyambua nyambua).

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ ﴿٥﴾

5. Na nini kitakujulisha ni nini hiyo Al-Hutwamah?

 

 

نَارُ اللَّـهِ الْمُوقَدَةُ ﴿٦﴾

6. Ni moto wa Allaah uliowashwa.

 

الَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى الْأَفْئِدَةِ ﴿٧﴾

7. Ambao unapanda nyoyoni.

 

 

إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ ﴿٨﴾

8. Hakika huo utafungiwa juu yao kila upande.

 

 

فِي عَمَدٍ مُّمَدَّدَةٍ ﴿٩﴾

9. Katika nguzo zilizonyooshwa.

 

 

 

Share