Kastadi Ya Boga Kwa Maziwa Na Lozi

Kastadi Ya Boga Kwa Maziwa Na Lozi

Vipimo 

Boga la kiasi - Nusu

Mdalasini - 1 kijiti

Maziwa -  2 gilasi mbili

Unga wa kastadi (custard powder) -  2 vijiko vya supu mfuto

Maziwa mazito (condensed) - ½ gilasi

Sukari -  ½ gilasi

Hiliki unga - 1 kijiko cha chai

Arki au vanilla - 1 kijiko cha chai

Lozi nyeupe - 1 kikombe                                                                                                  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   


  1. Roweka lozi utoe maganda ukatekate nyembamba au nunua za tayari


  2. Menya boga ukatekate vipande vya kiasi


  3. Weka boga katika sufuria, weka na kijiti cha mdalasini.


  4. Funika upike moto mdogo mdogo huku ukigeuzageuza mpaka litoke maji yake kidogo na lianze kuiva.


  5. Changanya kastadi (custard powder) katika kikombe na maji kidogo.


  6. Mimina maziwa, maziwa, sukari, na kastadi uliyochanganya na maji, endelea kupika mpaka liwive kabisa, huku liponde kidogo.


  7. Weka maziwa mazito (condensed), hiliki, arki au vanilla.

  8. Likiwa zito ongezea maziwa ya maji kidogo.

  9. Weka lozi


  10. Epua likwa tayari   

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

Share