Aiskrimu Ya Kokteli Ya Vanilla

Aiskrimu Ya  Kokteli Ya Vanilla  

 

Vipimo:

Tikiti maji (water melon)  -  ¼

Shammaam (tikiti, cantelope) -   ½

Papai -  1

Embe -  1

Peya (pear) -  2

Tofaha (apple) -  2

Machungwa -  2

Plamu (plums) -  3

Pichi (peaches)  -  3

Zabibu -  Kiasi

Tango - 1

Matunda yoyote mengineyo upendayo -  Kiasi

Aiskrimu ya vanilla - 1 L

 

Namna Ya Kutayarisha

  1. Menya matunda yanayohitaji kumenywa.

  2. Katakata matunda yote isipokuwa zabibu ikiwa ni ndogo ndogo. Ikiwa ni kubwa kubwa katakata pia.

  3. Changanya matunda yote vizuri katika bakuli kubwa.

  4. Teka kiasi weka katika gilasi.

  5. Chota (scoop) aiskrimu, weka juu ya matunda.

  6. Weka katika treya ikiwa tayari kuliwa.

Kidokezo:  

  1. Tumia matunda yoyote mengineyo upendayo.

  2. Kipimo hiki ni  kiasi cha gilasi 12 au zaidi.

 

 
Share