Biskuti Za 'Aynul-Jamal (Jicho La Ngamia)

Biskuti Za ‘Aynul-Jama Jicho La Ngamial

 

Vipimo

Unga ngano mweupe -  2 ½ vikombe

Unga wa mahindi/sembe -1 kikombe

Sukari laini kabisa (isage) -   1 kikombe

Baking powder -  ½ kijiko cha chai

Siagi laini  - 250 gms

Mayai - 2

Vanilla -1 kijiko cha chai

Chumvi  -  chembe

           

Unahitaji kuwa na mashine hasa ya kupikia biskuti hizi za 'aynul-jamal.

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

1-Changanya vizuri siagi, sukari kwa mchapo wa mkono kisha changanya mayai.

2-Tia pole pole unga na vilobakia uchanganye vizuri. Mchanganyiko usiwe laini sana yaani usiwe maji maji. 

3-Washa mashine ishike moto.

4-Kisha fanya vidonge vya round vidogodogo.

   
 

5- Weka vidonge katika mashine ya aynul-jamal.

6-Funika upike kiasi ya dakika 10 au chini yake.
 

7-Tumia kijiti kirefu cha mishkaki kutolea. Epua vibiskuti.

8-Rudia kumalizia kupika vidonge vyote.

9-Vikishapoa, jaza baina ya biskuti mbili kwa caramel au tofi ugandishe. Caramel au tofi zinapatikana katika viungo vifuatavyo:

Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream

Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito

10-Pangusa caramel iliyozidi kisha viweke kila kimoja katika kijikaratasi chake kama ilivyo katika picha juu, upange katika sahani ya kupakulia.

9-Ukipenda saga aina za njugu unyunyize pembezoni kama hivi.

Vidokezo:

1-Andaa caramel mapema kabla ya vibiskuti ipate kupoa

2-Unaweza kutumia sosi ya tayari inayouzwa katika chupa mfano ‘nutella’ badala ya kuandaa caramel.

3-Ukipenda kumtumia mtu hadiya au ukipenda kufanya biashara, unaweza kuzifunga na kuzipamba kama design zifuatazo.

4-Ukipenda kuzifanya za rangi mbali mbali  au za chokoleti, basi gawa unga usarifu upendavyo.

 

 

   

5-Caramel hizo za kuandaa mwenyewe unaweza kutumilia katika mapishi mengineyo kama keki, biscuit, kaimati, sharbaat n.k

 

 

Caramel Aina ya 3

 

Sukari ya brown (brown sugar) - 100 gms

Siagi - 100 gms

Cream au maziwa mazito -100 ml

 

1-Weka siagi na sukari katika sufuria ndogo au frying pan, weka katika moto ukoroge mpaka siagi na sukari iyayuke. Isiungue.  

2-Tia maziwa ya cream uendeleze katika moto itatoa povu, changanya na koroga vizuri usiache mkono. 

3-Epua ikiwa tayari ihifadhi katika chupa ya gilasi.

 

 

Share