Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream

Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream

Vipimo

Sukari - 1 kikombe

Maji - ¼ kikombe

Maziwa ya malai (whipping cream) -½ kikombe

Siagi - 1 kijiko cha kulia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika.

1-Weka sukari na maji katika sufuria kisha pika katika moto mdogo mdogo sana. ​Koroga usiachie mkono mpaka itoke mapovu

2-Ikianza kubadilika rangi ya brown epua.  Rangi ya brown upendavyo ukipenda iwe light au ikoze zaidi lakini isiungue.

3-Epua,mimina maziwa ya malai mazito (thick creamy milk au whipping cream)koroga vizuri

4-Tia kidonge cha siagi koroga kidogo katika moto.

5-Epua ipoe 

 

Vidokezo:

  1. Caramel unaweza kuhifadhi katika chupa ya gilasi utumie katika vitamu vinginevyo kama keki, pudding, kaimati, biskuti za 'aynul-jamal na nyenginezo na kadhaalika.
  2. Unaweza kutengeneza zaidi ya mara moja kuhifadhi kwa wingi.     

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

Share