Tambi Za Nazi Za Sukari Ya Brown

Tambi Za Nazi Za Sukari Ya Brown

Vipimo

Tambi nyepe za mchele - 1 paketi

Tui la nazi zito - 2 gilasi

Sukari ya brown - ¾ gilasi

Maziwa ya unga - 3 vijiko vya kulia

Samli - 2 vijiko vya kulia

Hiliki - 1 kijiko cha chai

Zabibu - ¼ gilasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni. Paka siagi treya ya oven.
  2. Weka maji ya moto katika sufuria yakianza kuchemka weka tambi ulizokatakata kisha zitoe haraka zisichemkie sana humo. Zimwage maji uchuje.
  3. Changanya tui, samli, maziwa, hiliki katika kibakuli.
  4. Mwagia sukari ya brown katika treya ya oveni.
  5. Weka tambi kisha mwagia zabibu. Kisha tia mchanganyiko wa tui uchanganye vizuri. 
  6. Oka (bake) huku ukichanganyachanganya.
  7. Tui likikauka, epua pakua katika sanahi zikiwa tayari.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

Share