Kaimati Aina Ya 4 Za Shira Tende Na Sukari

                            

Kaimati Aina Ya 4 Za Shira Tende Na Sukari

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Unga - 1 kikombe kikubwa (mug)

Hamira - 1 ½

Mafuta - 1 kijiko cha supu    

Mtindi (yoghurt) - 1 kijiko cha supu

Maji - 1 kikombe kimoja takriban

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katika bakuli weka, unga, hamira (ikiwa ya instant, ama ikiwa ya chenga uumua pekee katika kikombe kidogo kwa kuweka nusu kijiko sukari na maji kidogo)
  2. Weka vitu vilobakia kisha changanya vizuri uchanganyike uwe mlaini.
  3. Funika uumuke. Ukishauumuka (ukishafura) choma katika mafuta ya moto mpaka zigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
  4. Epua zichuje mafuta.
  5. Gawa sehemu mbili; sehemu utie shira ya tende inayouzwa tayari madukani, na sehemu uti shira unayotengeneza mwenyewe nyumbani.
  6. Nyunyizia ufuta ukipenda.

Shira

Sukari - 2 kikombe

Maji - 1 kikombe

Hiliki

Arkii (rose flavor)

Namna Ya Kutengeneza Shira

  1. Changanya weka katika moto mdogomdogo, ipike ichemke pole pole.
  2. Tia hiliki, arki (rose flavor)
  3. Tumia kiasi, itakayobakia iihifadhi katika chupa ya gilasi.

 

 

Share