Basbusa Za Nazi Mtindi Na Njugu Mchanganyiko (Shaam)

Basbusa Za Nazi Mtindi Na Njugu Mchanganyiko

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Unga wa semolina (mahindi wa chenga) - 2 vikombe

Nazi ya chenga kavu - 1 kikombe

Samli - ½ kikombe

Mtindi (yoghurt) - 1 kikombe

Sukari - ¼ kikombe

Baking soda - 1 kijiko cha chai

Vanilla - 1 kijiko cha chai

 

Shira:

Sukari - 2 vikombe

Maji - 1 kikombe

Zaafarani au flavour yake, au flavour ya rose - matone kiasi

Ndimu ya maji - 1 kijiko cha chai                                                                                                                            

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

 1. Tayarisha kwanza shira yake iache ipoe.
 2. Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa njugu.
 3. Funika bakuli uwache kwa muda wa saa moja takriban.
 4. Changanya tena, kisha fanya viduara vya kiasi.
 5. Washa oveni mapema.
 6. Weka katika treya uliyopaka siagi.
 7. Nyunyizia njugu ulizokatakata (chopped)
 8. Tia katika oven moto wa kiasia 300- 400 degrees. Uchome (bake) kwa nusu saa zigeuke rangi.
 9. Epua kisha mwagia shira yake iliyo baridi ipate kuingia mpaka ndani ya basbusa.
 10. Vitoe na upange  katika sahani ya kupakulia.

Kutengeneza Shira

 1. Weka vitu vyote katika kisufuria uchemeshe katika moto mdogo mdogo, mpaka iwe nzito kiasi.
 2. Epua ipoe.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

Share