Trifle ya Tambi Jelly Na Ice cream Ya Vanilla

  Trifle Ya Tambi Jelly Na Ice cream Ya Vanilla

 

  

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo 

Tambi nyembamba - 2 vikombe viwili

Jelly ya strawberry au raspberry - 2 paketi

Mchanganyiko wa fruit (fruit cockatil) - 1 kibati kikubwa

Ice cream ya vanilla                                                         

Sharbati ya rosy (rose syrup)    

                                                

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

1-Tengeneza jelly kama yalivyo maelezo katika paketi zake lakini ifanye nzito zaidi kwa kupunguza maji kidogo.  Iache igande katika friji.

2-Weka maji ya moto, yakichemka tia tambi zichemke mchemko wa chini ya dakika moja. Tia siagi kidogo au mafuta. . Epua uchuje maji. Mwagia maji ya baridi kidogo ili zisigande.  

3-Tayarisha gilasi za kupakulia.  

4-Katakata jelly vipande  vidogodogo vya mraba (square)

5-Chota tambi kidogo weka katika gilasi

6-Chota jelly weka juu ya tambi.

7-Weka mchanganyiko wa fruit.

8-Teka miteko miwili ya icecream weka juu

9-Mwagia sharbati ya rose kiasi

10-Weka gilasi zote katika treya na vijiko vyake ikiwa tayari. 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share