Trifle Ya Mchanganyiko Wa Furusadi (Berries)

Trifle Ya Mchanganyiko Wa Furusadi (Berries) 

   

Vipimo Vya Kastadi 

Viinimayai (egg yolks) -  4 

Sukari - ½ kikombe 

Unga wa mahindi mlaini (corn starch) - 2 vijiko vya chai 

Malai mazito (double cream) - 2 vikombe 

Vanilla -  2 vijiko vya chai  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kastadi 

 1. Katika bakuli, piga kwa   mchapo wa mayai  (egg Whip) viini vya mayai, sukari na unga wa mahindi hadi iwe laini na kuchanganyika vizuri.
 2. Mimina malai katika kisufuria kidogo weka katika moto wa kiasi na yaache hadi karibu na kuchemka.
 3. Polepole yamimine katika mchanganyko wa mayai huku ukiendelea kupiga kwa mchapo bila ya kusita hadi ichemke kiasi na iwe nzito
 4. Rudisha mchanganyiko katika sufuria na pika katika moto wa kiasi mdogo kama dakika 4.
 5. Mimina katika bakuli jengine, tia vanilla,   changanya.
 6. Funika vizuri kabisa kwa karatasi ya plastiki ya kufunikia (Plastic wrap) ili hewa isiingie na kusababisha kufanyika ngozi.
 7. Weka katika friji hadi iwe baridi kwa muda wa masaa 2 au hata tokea usiku.  

Vipimo Vya Mjazo Wa Beri   

Furusadi changanyiko ya beri (blue berries,

Stroberi, raspberries n.k.) -  6 vikombe 

Ndimu - 1  kijiko cha supu 

Slesi za keki - 6 

Juisi nzito ya nanasi au chungwa - 3 vijiko vya supu   

Namna Ya Kutayarisha Mchanganyiko Wa Berries 

Katika bakuli jengine, tia furusadi  zote, tia 2 vijiko viwili vya sukari, ndimu, juisi vijiko 3 uchanganye vizuri.  Weka kando. 

Vya Kunyunyuzia  

1-Malai matamu yaliyopigwa na wiski (whipped sweetened cream)

2-Lozi zilizokatwakatwa  

Namna Ya Kuitayarisha Trifle  

 1. Panga slesi 3 kwanza za keki katika bakulia la kupakulia.
 2. Mimina juu yake nusu ya mchanganyiko wa furusadi na ya nusu juisi yake.
 3. Mimina nusu ya mchanganyiko wa kastadi.
 4. Rudia tena kuweka slesi za keki zilobakia, miminia mchanganyiko wa berries na juisi yake, mimina kastadi iliyobakia, kisha rudisha katika friji kwa muda wa masaa kama 4 au zaidi.
 5. Wakati wa kupakua mwagia malai matamu yaliyopigwa wiski (Whipped cream), na nyunyizia na lozi.  

         

Kidokezo: 

Wakati wa kutayarisha Trifle, unaweza kugawa mchanganyiko huo ukipenda katika vigilasi au vibakuli mbali mbali badala ya kufanya katika bakuli moja kubwa

 

 

 

Share