Pudini Ya Sago (Pakistani)

Pudini Ya Sago

 

   

 

 

Vipimo

 

Sago - ½ kikombe

Maji - 1 ½ kikombe

Maziwa - 2 gilasi

Sukari -  ½ kikombe  takriban

Hiliki ya unga -  ½ kijiko cha chai

Zaafarani roweka katika maji -  ½ kikombe cha kahawa                          

Au tumia flavour ya zaafarani ya tayari -  5 – 7 matone

Lozi, njugu za pistachio -  ½ kikombe                                     

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Roweka chembe za sago katika maji kiasi cha dakika 25- 30 (kila ukiroweka zaidi utapunguza muda wa kuchemsha)

  1. Chemsha maji kisha mimina chembe za sago ukoroge mpaka igeuke kuwa nzito.
  2. Tia maziwa uendelea kukoroga ichemke kiasi huku ikiwa nzito kama vile uzito wa kastadi kabla ya kuganda.
  3. Tia sukari kiasi upendacho ukoroge.
  4. Tia zaafarani uloroweka au flavour yake, au flavour ya rose, na tia hiliki.
  5. Mimina katika bakuli kisha pambia lozi na njugu za pistachio au njugu upendazo zisizokuwa za chumvi
  6. Kulia na jelly ya ndimu au yeyote upendayo utayarishe kama ilivyoandikiwa katika paketi.

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

 

Share