Mboga Mchanganyiko Ya Kukaanga Na Uyoga Kwa Sosi ya Soya

Mboga Mchanganyiko Ya Kukaanga Na Uyoga Kwa Sosi ya Soya

 

Vipimo 

Bakuli la kwanza:

Kitunguu kilokatwakatwa slesi - 1

Tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha kulia

Thomu (garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha kulia

Karoti ilokatwa slesi nyembamba -  1

Uyoga (mushrooms) katakata vipande vipande - 1 kikombe

Koliflawa (cauliflower) katakata - ¼  ya uwa moja

Bakuli la pili:

Njegere za kijani (green peas) - 1 kikombe

Maharage ya kijani - 1 kikombe kimoja

Brokoli (broccoli)   katakata vipande - ½ ya uwa moja

Figili mwitu (celery) katakata - 1 mche  

Vinginevyo:

Sosi ya soya (soy sauce) - 3 vijiko vya kulia

Sukari - 1 kijiko cha chai

Unga wa mahindi mlaini (Corn starch)  - 1 kijiko cha chai

Kidonge cha supu - 1

Mafuta -  3 vijiko cha kulia

                                   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Weka karai la kukaangia mboga (Wok) katika moto, tia mafuta yashike moto.
  2. Mimina vitu katika bakuli la kwanza, ukaange na ukoroge katika moto wa kiasi mpaka mboga zake humo ziive nusu yake. (kiasi dakika 3)
  3. Weka sosi ya soya, sukari, kidonge cha supu changanya vizuri ibakie motoni kiasi dakika moja
  4. Mimina vitu vya bakuli la pili na korogoa. Acha vipikike kiasi dakika 2.
  5. Katika kibakuli kidogo, weka cornstarch utie maji kiasi kijiko kimoja cha kulia uchagane vizuri.  Tia katika mboga. Zima moto, kisha pakua katika sahani utie juu yake vitunguu vya majani (springi onions) au chives (aina ya vitunguu kama spring onions) au dill (aina ya kotmiri mwitu)

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share