Mchicha Na Karoti Kwa Supu Ya Nyama

Mchicha Na Karoti Kwa Supu Ya Nyama  

 

Vipimo

Mchicha - 2 Misongo

 Karoti katakata - 2

Kitunguu katakata - 1

Nyanya katakata - 2

Nyanya sosi (tomato paste) - 2 vijiko vya supu

Supu ya nyama ng’ombe - 1 kikombe au kidonge kimoja

Siagi au mafuta - 3 vijiko vya supu

Pilipili manga (black pepper) - ¼ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

 Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

1.      Osha mboga vizuri, katakata uchuje maji.

2.      Weka siagi katika sufuria, kaanga vitunguu viwe laini kisha tia nyanya, kaanga.

3.      Tia nyanya kopo kaanga, tia chumvi na pilipili manga.

4.      Tia supu, kisha tia karoti na mchicha acha ipikike muda kiasi tu.

5.      Epua uweke katika bakuli ikiwa tayari, tolea na wali mweupe.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share