Nyanya Za Mshumaa/Chungu/Ngogwe Za Kukaanga

Nyanya Za Mshumaa/Chungu/Ngogwe Za Kukaanga

   

Vipimo

Nyanya za mshumaa/chungu - 20 kiasi

Kitunguu - 1

Nyanya/tungule - 2

Mafuta ya zaytuni (olive oil) - 3 vijiko vya supu

Pilipili mbichi - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) -  3 chembe

Chumvi -  kiasi 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Osha  nyanya za mshumaa/chungu kisha zichemshe kidogo.        

        

  1. Mwaga maji, menya maganda na ukatekate vipande vipande. 
  2. Katakata kitunguu, nyanya vipande vidogovidogo (chopped) 
  3. Saga au katakata pilipili mbichi na thomu. 
  4. Weka mafuta katika sufuria, tia vitu vyote pamoja. Kaanga kwa muda huku unakoroga hadi iwive.  
  5. Pakuwa katika chombo, nyunyizia mafuta ya zaytuni.

 

 

 

 

 

 

Share