Mboga Mchanganyiko Ya Kuchemsha (Steamed) Kwa Supu.

Mboga Mchanganyiko Ya Kuchemsha (Steamed) Kwa Supu.

    

Vipimo

Viazi - 2

Pilipili kubwa (capsicum) ya kijani - 1

Pilipili kubwa (capsicum) ya rangi orengi au manjano - 1

Brokoli (brocoli) - 1 mshikano (bunch)

Karoti - 2

Koliflawa (cauliflower) - ¼ ya uwa zima

Pilipili manga

Kidonge cha supu (stock) ya nyama ng’ombe  - 1

Chumvi - Kiasi

Maji - 1 kikombe

Namna Ya Kupika:  

  1. Changanya pamoja katika sufuria mboga zote pamoja. 
  2. Pasha maji yamoto weka katika kibakuli kidogo, changanya na kidonge cha supu koroga hadi iyayuke iwe supu.  
  3. Tia pilipili manga, chumvi, funika upike moto mdogo mdogo hadi mboga zikaribie kuiva  kwa mvuke. 
  4. Epua tayari  

 Kidokezo: 

Ikiwa huna kidonge cha supu, chemsha mifupa ya nyama ng’ombe utumie supu yake.

 

 

 

 

Share