Polourie Bajia Za Unga Dengu Na Mweupe (Trinidad)

Polourie Bajia Za Unga Dengu Na Mweupe (Trinidad)

Vipimo

Unga wa dengu -1 ½

Unga mweupe - 1 ½

Hamira - 1 ½ kijiko cha chai

Baking powder - 1 kijiko cha chai

Thomu (garlic/saumu) - 1 kijiko cha chai

Haldi (bizari ya manjano turmeric) - ½  kijiko cha chai

Samli - 2 vijiko vya chai

Chumvi - kiasi

Kotmiri ilokatwakatwa - mche mmoja kiasi ijae kikombe

Maji ya kutosheleza kuchanganya

Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Weka vitu vyote pamoja katika bakuli kisha changanya vizuri.
  2. Acha uumuke.
  3. Teka mteko wa round ndogo ndogo kama vikaimati utumbukize katika mafuta ukaange. Zikegeuka rangi kidogo tu, epua uchuje mafuta. Usikaange sana zisijekuwa ngumu.
  4. Kisha weka katika sahani zikiwa tayari. Tolea kwa sosi ya ukwaju. Bonyeza link upate upishi wa sosi ya ukwaju.

  Sosi Ya Ukwaju

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share