Imaam Ibn Al-Qayyim: Elimu Ni Funguo Za Furaha; Elimu Ya Kumjua Allaah Ni Msingi Wa Elimu Zote

 

Elimu Ni Funguo Za Furaha Duniani Na Aakhirah

 

Elimu Ya Kumjua Allaah Ni Msingi Wa Elimu Zote

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Imaam Ibn Al-Qayyim Al-Jawziyy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

"Elimu ya (kumjua) Allaah ni msingi wa elimu zote na ni msingi wa elimu ya mja ambayo inampatia furaha na ukamilifu na manufaa ya uhai wake wa dunia na uhai wa  wa Aakhirah yake. 

 

Na ujinga wa kutokuwa na elimu ya Allaah unapelekea ujinga kwa mtu na hata manufaa yanayopatikana na ukamilifu wake, hauwezi kuwa na faida wala mafanikio.

 

Hivyo basi, elimu Yake (Allaah) ni furaha ya mja na ujinga wake (wa kutomjua Allaah) ni asili ya kukosa furaha yake."

 

 

[Miftaah Daar As-Sa’aadah (239/1)]

 

 

 

Share