Kuongeza Pesa Kwa Niaba Ya Riba Iiliyobaki Benki

 

SWALI:

 nimeona humu majibu ya RIBA zile zinazotiwa ktk benki sasa nataka ufafanuzi,unatakiwa pesa zile usizitumie na uzitowe sadaka na sadaka hiyo haina malipo,sasa mfano ndio imetiwa labda centi ktk account na huwezi kutowa centi ile ile sasa unaweza kutowa kiwango kadhaa cha fedha halafu ktk hizo ukatowa ile sehemu ya RIBA ulotiliwa au ukatowa zaidi ya hiyo centi kufidia ile RIBA pale je hii inakubalika? au pengine zile pesa umeziweka mule hutaki kuzitowa sasa lakini unakiakiba chengine pembeni hutowi ktka account ile ulotiliwa RIBA je hapo naweza kutowa?

 

 


 

JIBU

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa du'aa zenu nzuri mnazotuombea nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia ALHIDAAYA kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah (Subhaana wa Ta'aala)   Atutakabalie hizo du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelimishana kwa kadiri Anavyotujaalia. Aamiyn

Kuhusu mas-ala haya yapo wazi kabisa. Hakika ni kuwa Muislam hafai kuchukua Riba lakini kwa madhara ambayo yamefanyika mbeleni kwa Waislam kuacha kwa benki ambazo si za Kiislam ni kuwa zinatumika kuipiga vita Uislam. Ili kuondosha madhara hayo Muislam anafaa achukue kisha aitoe kwa kujenga vyoo, kusaidia karo za Waislam masikini na misaada mingineyo. Ikiwa huwezi kutoa senti basi ni bora utoe nyingi kidogo kuliko ilivyo katika nyaraka za kutoka benki. Mfano riba yenyewe ni shillingi 1546.15, senti 15 kwa siku hizi hazipo kwa hivyo itakuwa ni bora wewe utoe 1547 au hata 1550 hizo za ziada zitakuwa ni sadaka kwa upande wako.

 

Kuhusu kuitoa kabisa kutoka benki kiwango hicho ili uitoe kwa msaada ambao umedhamiria. Hakika ni bora zaidi kuitoa kutoka katika benki kiwango hicho lakini ikiwa una kiakiba pembeni kutakuwa hakuna shida yoyote. Hivyo, ni mas-ala ya ubora lakini zote zinafaa.

Na Allah Anajua zaidi

 

 

Share