Donuts Za Kumwagiwa Chokoleti Juu Na Icing Sugar

Donuts Za Kumwagiwa Chokoleti Juu Na Icing Sugar

 

 

Vipimo 

 

Unga vikombe 3

Hamira kijiko 1 ½ cha kulia

Maziwa vijiko 2 vya kulia

Siagi 2 vijiko 2 vya kulia

Sukari vijiko 3 vya kulia

Chumvi ½ kijiko cha chai

Kiasi 1 cha kiasi chemsha sana uponde kiwe laini.  

Maji ya vuguvugu (warm)

 

 

Mafuta ya kukaangia

Icing sugar na syrup ya chokoleti ya tayari kwa ajili ya kunyunyuzia

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Changanya vitu vyote katika bakuli isipokuwa maji. Changanya vizuri.
  2. Polepole tia maji uchanganye kisha ukande upate donge laini lisiloganda mkononi.
  3. Liache donge liumuke kiasi ya ¾ au saa moja.
  4. Sikuma donge kisha katakata round kutumia gilasi ndogo.
  5. Fanya kishimo katika kila duara unalokata kwa kutumia kifuniko cha chupa.

  1. Choma (kaanga) katika mafuta kwenye karai yaliyoshika moto kisha epua uchuje mafuta.
  2. Saga sukari au tumie icing sugar unyunyuzie baadhi ya donuts na baadhi nyunyuzia syrup ya chokoleti ya tayari.
  3. Ukipenda nyunyuzia visukari vya rangi rangi kwa ajili ya watoto.

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

Kidokezo:  Viduara ulivyokatia kifuniko cha chupa unaweza kuunda duara nyengine au vikaange kama vilivyo.

Share