Imaam Ibn Baaz: Kuegesha Kengele Ya Saa Ikuamshe Baada Jua Kuchomoza Ukapitwa Swalaah Ni Kufru

Kuegesha Kengele Ya Saa Ikuamshe Baada Jua Kuchomoza Na Kupitwa Swalaah Ni Kufru

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Yeyote atakayeegesha kengele ya saa makusudi imuamshe baada ya kutoka jua akakosa Swalaah ya Alfajiri, basi mtu huyo amepuuza kuswali kwa wakati wake na hivyo ni kufru kubwa kama walivyokubaliana ‘Ulamaa wengi kwa sababu amekusudia kuswali baada ya jua kutoka. Ni sawa na mtu ambaye anachelewesha kuswali Alfajiri akaiswali karibu na Adhuhuri.

 

 

[Fataawa Ibn Baaz, Kitaab As-Swalaah 10/374].

 

Share