Shaykh Fawzaan: Kwanini Salaf Wametahadharisha Qaswaswuwn (Wahadhiri Wapendao Kutumia Visa Vya Uongo)

 

Kwanini Salaf Wametahadharisha Qaswaswuwn (Wahadhiri Wapendao Kutumia Visa (Vya Uongo) Katika Ulinganiaji?

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

SWALI:

 

Salaf wamewataja wenye kupenda kutoa visa na wakawalaumu. Je, vipi njia zao na nini inatuwajibikia sisi kuhusu wao?

 

 

JIBU:

 

Salaf (Rahimahumu Allaah) wamehadharisha kuhusu Qaswaswuwn (wahadhiri wanaopenda kutoa visa ambavyo aghlabu ni vya uongo) kwa sababu aghlabu hawakusudii katika mazungumzo yao isipokuwa yale ya kuleta taathira kwa watu kwa vile visa ambavyo havijasihi (si sahihi). Wala hawategemei dalili sahihi, wala hawahimizi kufundisha watu hukmu (shariy’ah) za Dini yao na mambo ya ‘Aqiydah yao kwa sababu hawana 'ilmu ya shariy'ah.

 

 

[Al-Ajwibatu Al-Mufiydah ‘An As-ilah Al-Manaahij Al-Jadiydah (Uk.244)]

 

 

Na Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) ana majibu yanayofanana na hayo katika sehemu nyingine na yenye ziada ifuatayo:

 

"Wamehadharisha (Salaf) kuhusiana na Qaswaswuwn (wanaopenda kutoa visa aghlabu vya uongo), yaani watoaji waadhi, kwa sababu wanataka kuwaathiri (kuwavutia) watu, hawatafuti uthabiti wa visa na khabari (masimulizi) wanayosimulia, wanakuja na kila wanachokisoma bila kuthibitishi. Na wanataja Ahaadiyth ambazo zinakuwa ni za kutungwa au dhaifu, wala hawafanyii uthibitisho (hawafanyi utafiti kuhakikisha usahihi wa wanayosimulia), kwa sababu hamu yao kuu ni kuwaathiri watu (kuwavutia na kuwasisimua).

Kwa hali hiyo, ndio sababu Salaf wakawahadharisha watu kuhusu wapiga visa (porojo) kwa sababu hawafanyii uthibitisho masimulizi wanayosimulia...Na'am.

 

Share