Sha'baan: Uzushi Niswfu Sha'baan Na Kuhusu Qismatu Rizq (Mgawanyo Wa Rizki)

 

 

Uzushi Niswfu Sha'baan Na Kuhusu Qismatu Rizq (Mgawanyo Wa Rizki)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalaamu Alaykum ndugu zangu.

 

Naomba kuwauliza nisaidieni tafadhali. Kuna forwards katika mitandao ya kijamii kuhusu Sala inayosaliwa kuomba du’aa ya  kasmati rizki katika mwezi wa Shaabani. Kisha kuna watu na watoto wanapita majumbani kugawa vyakula na pipi na kuomba pesa wakisema kuwa ni usiku wa kasmati rizki, je ni sahihi?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.  

 

 

Hakuna Swalaah wala ‘ibaadah yoyote ile iliyothibiti ya mtu kupata riziki au kugaiwa riziki kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).  Kila mtu anapozaliwa huwa ashaandikiwa riziki na umri atakaoishi hapa duniani. Kwa hivyo kuomba du’aa wakati wa nusu ya Sha'baan haipo katika Uislaam kabisa.

 

 

Kugawa vyakula majumbani ni usiku wa Niswfu Sha'baan mtindo wa Mashia huo na hujulikana kwao pia kwa “Haqqul-Laylah” (Haki ya usiku). Hakika huu ni uzushi na kuingilia hukmu za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika swala la ugawaji wa rizki ambao hakuna mwenye uwezo nao isipokuwa Yeye Mwenyewe Pekee (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

 

Kwa faida ziyada, bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Uzushi Wa Mashia Wa Swalah Ya Usiku Wa Mwanzo Wa Sha'baan

 

Kufunga Na Kukutanika Usiku Wa Niswf Sha’baan Na Kufanya Kisomo Inafaa?

 

Fatwa: Shaykh Swaalih Al-Fawzaan - Hakujasihi Chochote Kuhusu Niswf Sha'baan

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

 

 

 

Share