Parfait Ya Embe Mtindi Wa Fruti Malai Na Biskuti

Parfait Ya Embe Mtindi Wa Fruti Malai Na Biskuti

 

 

Vipimo

 

Embe ziloiva tamu - 2

Biskuti za aina ya digestive -  5

Malai (cream) - vijiko 3 vya kulia

Mtindi wa kigiriki – vijiko 3 vya kulia

Mtindi wa embe au wa fruti yeyote ile-  kikombe 1

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Weka katika bakuli, mtindi wa embe au wa fruti yeyote ile upendayo, mtindi wa kigiriki uchanganye vizuri.
  2. Ponda biskuti.
  3. Weka katika vigilasi tabaka ya biskuti.
  4. Weka tabaka ya mchanganyiko wa mtindi.
  5. Menya embe zote mbilie.
  6. Weka embe moja uisage katika mashine ya kusagia (blender) mpaka iwe rojo. Kisha tia katika vigilasi kuweka tabaka ya tatu.
  7. Embe ya pili, ikatekate vipande vidogo dogo kisha tia kwa kugawa katika vigilasi kama tabaka ya mwisho.
  8. Weka katika friji kwa muda upendao ikiwa tayari.

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

Share