Shaykh Fawzaan: Kuelekea Qiblah Wakati Wa Kusoma Qur-aan

 

Kuelekea Qiblah Wakati Wa Kusoma Qur-aan

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Je, inawajibika kuelekea Qiblah wakati wa kusoma Qur-aan?

 

 

JIBU:

 

Inapasa kuelekea Qiblah kwa sababu kusoma Qur-aan ni ‘ibaadah, na ‘ibaadah inapendekezwa kuilekeza Qiblah. Basi ikiwezekana hivyo itakuwa ni katika ukamilifu (wa kutekeleza ‘ibaadah), lakini ikiwa hakuweza mtu kuelekea Qiblah basi hakuna ubaya.

 

 

[Al-Muntaqaa Min Fataawaa Ash-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (2/35)]

 

 

Share