Mkate Wa Sinia - Mkate Wa Kumimina -1

 


 


 

Vipimo

     ·        1 KIKOMBE CHA MCHELE

 

·        1 KIKOMBE CHA NAZI YA UNGA 

·        1 KIKOMBE CHA SUKARI KUPUNGUA KIDOGO

·        1 KIKOMBE CHA MAJI AU MAZIWA VUGUVUGU

·        1 KIJIKO CHA CHAI CHA HAMIRA

·        ILIKI KIASI UPENDAVYO

·        UTE WA YAI MOJA

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kulpika

1.  Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.

2.  Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka  mchanganyiko uwe lani kabisa. 

3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).

4.  Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.

5. Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.

6.  Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.

7.  Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata. Ni bora kuula siku ya pili yake.

 

Share

Comments

3

Useful site where i could learn a lot in religion and cookery as well.

god bless for people who open this website thank you nimefurahi sana kufungua web hii na kupata vitu nipendavyo , kwani ni siku nyingi nataka kujua jinsi ya kupika mate wa kumimkina
THANX

My taste buds can't wait to eat Mkate ya Siniya! But I would appreciate the recipe to be translated to English. I have eaten it in Mombasa. Please...God Bless.