Buns Tamu Za Siagi

Buns Tamu Za Siagi

 

Vipimo   

 

Unga gilasi 3

Siagi vijiko 4 – 5 vya kulia

Sukari ½  kikombe

Maziwa kikombe 1

Maji kikombe 1 ¼

Hamira kijiko 1 cha chai

Yai 1

Mtindi (yoghurt/maziwa lala) kijiko 1 cha kulia

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Tia vitu vyote katika bakuli uchanganye vizuri, kisha ukande unga uwe mlaini.
  2. Funika kwa karatasi ya jalbosi kwa dakika chache uumuke.
  3. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi.
  4. Nyunyizia ufuta.
  5. Pika (bake) katika oven moto wa kiasi mpaka vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown)
  6. Epua buns zikiwa tayari.

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share