Koni Za Tuna Na Salad

Koni Za Tuna Na Salad

Vipimo vya Unga

Kupata Koni 40

Unga - Gilasi 4

Mafuta -  ¼  Gilasi

Maziwa ya unga - Vijiko 4 vya chakula

Sukari -  1 Kijiko cha chakula

Chumvi - 1 Kijiko cha chakula

Baking powder - Kijiko cha chai

Hamira - 1 Kijiko cha chakula

Vipimo vya saladi

Saladi ya duara iliyokatwakatwa -  1/2

Karoti zilizokwaruzwa - 2

Mahindi matamu yaliyokwishapikwa - 1 kikombe cha chai

Vikopo vya tuna - 3

Mayonnaise  - 2 vijiko vya chakula

Pili pili manga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi 

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Kanda unga  kwa kutumia vitu vyote.
  2. Ukishachanganyika vizuri, acha uumuke.
  3. Kata madonge ya duara kama ya chapati.
  4.  Sukuma kisha kata vipande virefu virefu vya mstatili.(rectangle)
  5. Kunja kwenye chuma kama kwenye picha na panga katika treya ya kupikia. 

     6. Paka maziwa ya chai juu yake.

     7. Zitie kwenye jiko na uzipike (bake) kwa moto wa 350 Deg kwa muda wa dakika 20 mpaka ziwive na zigeuke rangi.

     8. Epua toa vyuma, weka kando. Ikiwa huna vyuma vilivyotimia 40 itabidi kila ukimaliza kupika ulivyonavyo, utoe vyuma utumie tena kuzungushia unga na upike hivyo hivyo hadi umalize unga wote.  

     9. Changanya vitu vya saladi vyote katika bakuli.

    10. Tumia kijiko kidogo, teka saladi na ujaze ndani ya koni kisha zipange katika  sahani ya kupakulia zikiwa tayari kuliwa.

Kidokezo:

Unaweza kujaza chochote upendacho badala ya saladi ya tuna, kama mfano kuku, nyama ya kusaga, hata vitu vitamu kama chokoleti. 

Vyuma hivyo vya koni vinapatikana nchi za Arabuni na Tanzania.

 

 

 

 

 

 

Share