Pizza

VIPIMO:
Unga 4 Vikombe
Maziwa ya unga 2 vijiko vya supu
Mafuta ya zaituni ½ kikombe
Hamira 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Sukari 1 kijiko cha chai
Maji dafu dafu 2 kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga.
2. Ufunike na uache uumuke.
SOSI YA PIZZA
Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo 1
Thomu iliyokatwa ndogo ndogo 3 chembe
Sosi ya HP 3 vijiko vya supu
Sosi ya tomato 3 vijiko vya supu
Pilipili manga 1 kijiko cha chai
Oregano ½ kijiko cha chai
Parsley (ukipenda) ½ ukipenda
1. Kaanga vitunguu kisha tia thomu, na vitu vyote iwe sosi.
2. Epua kwenye moto.
UPENDAVYO KATIKA HIVI AU VYOVYOTE VINGINEVYO
Tuna
Nyama ya kusaga iliyopikwa
Kuku aliyekaushwa na kukatwa vipande vipande
Sauage zilizokatwa
Salami
Vipande vya nanasi
VITU VYA KUJAZA JUU YA PIZZA
Nyanya zilizokatwa vipande vipande
Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo
Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi
Cheese ya Mazorella
1. Fanya madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu size
2. Paka sosi juu ya unga
3. Tia kiteo upendacho
4. Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza
5. Mwagia cheese
6. Pika katika oveni kwa muda dakika 20 au zaidi hadi ziwive pizza.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



As-salaam Aleikum Jazakum
As-salaam Aleikum
Jazakum Allah kheirun kwa kazi yenu.
Tafadhali nieleze- maji dafu dafu ni maji ya aina gani ?
Shukraan
Assalaamu 'alaykum
Assalaamu 'alaykum
Tunatumai pia unafaidika na chakula cha moyo ambacho ni Qur-aan, Mawaidha, Makala n.k.
Maji ya dafudafu ina maana ni maji yamotomoto (warm)
Jazaakumu Allaahu Khayra