Pizza Ya Viazi

Pizza Ya Viazi

 

Vipimo

Unga wa ngano - 3 Vikombe vya chai

Chumvi - 1 1/2 Kijiko cha chai

Sukari - 3/4 Kijiko cha chai

Maji - 1 3/4 Vikombe vya chai

Hamira - 1 Kijiko cha chai kilichojaa

Viazi - 2 Vikubwa

Kitungu - 1 kidogo

Mafuta ya Zeituni - 4 Vijiko vya supu

Namna ya kutengeneza na kupika

  1. Changanya unga, 1/2 kijiko cha chai chumvi, sukari, na hamira katika mashine,na mimina maji pole pole.Uwache unga ukandike vizuri hadi ilainike.
  2. Ufunike na uache uumuke kwa masaa 2 au zaidi.
  3. Tayarisha viazi kwa kuzikata slesi na kuziroweka ndani ya maji ya baridi ili  isigeuke rangi.
  4. Kisha mwaga maji na uweke chumvi 1/2 kijiko cha chai, iwache kwa dakika 5 hivi ili itowe maji na uyamwage.
  5. Kisha changanya viazi, kitungu kilichokatwa, na mafuta ya zeituni kijiko 1, nauweke kando.
  6.  Washa oveni moto wa 440F.Tayarisha trei ya kuchomea kwa kuipaka mafuta.Kisha tandaza unga (uliokwisha fura), ukitumia mikono yako na kusambaza hadi pembeni mwa trei.
  7. Panga viazi, nyunyiza chumvi 1/2 kijiko cha chai, pilipili manga ya unga na mafuta ya zeituni vijiko 3 iliyobakia.
  8. Pika hadi pizza iwachane pembeni na kuwa rangi ya dhahabu, kama dakika 30 hivi.
  9. Epua, na iwache ipowe kidogo;kata vipande na itakuwa tayari kuliwa. 
Share