Croissant Tamu Za Kunyunyuziwa Ufuta

Croissant Tamu Za Kunyunyuziwa Ufuta

  

Vipimo 

Unga -  3 ¾ vikombe

Maji dafudafu (warm) - ½ kikombe

Maziwa dafudafu -  ½ kikombe

Yai -  1

Siagi (butter) - 1/3 kikombe

Sukari -  1/3 kikombe

Hamira - 2 vijiko vya chai

Siagi (nyengine) -  ¼ kikombe

Chumvi -  1 kijiko cha chai                                                      

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika    

 1. Changanya maji dafudafu (warm) pamoja na maziwa katika bakuli.
 2. Tia sukari ukoroge mpaka iyayuke.
 3. Weka hamira, acha kiasi dakika 10 mpaka ibadilike kuwa kama povu.  
 4. Piga yai utie humo, pamoja na siagi ya 1/3 na chumvi.
 5. Tia unga kidogo kidogo katika mchanganyiko wa hamira.
 6. Kanda kisha acha uumuke kiasi dakika 45 uwe size ya mara mbili yake.
 7. Gawa unga katika vidonge, kisha acha vidonge viuumuke tena kidogo.
 8. Sukuma kisha pakaza juu yake  siagi katika ile ya ¼ kikombe.
 9. Kunja katika shepu ya croissants kwa kukata katika shepu ya ncha tatu (triangle) kisha zungusha unga kuanzia upande ulio mpana kuelekea upande mdogo. 
 10. Panga katika treya ya kuchomea (bake). Nyunyizia ufuta kisha acha ziuumuke.
 11. Pakaza yai kwa brush, kisha pika katika oveni uoke (bake) mpaka zibadilike rangi na ziwive.

Vidokezo: 

 1. Washa oveni mapema
 2. Unaweza kufanya shepu yoyote upendavyo.
 3. Unaweza kujaza mjazo wowote kama wa kuku, jibini (cheese) na kadhaalika

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

Share