Kabaab Za Kuchoma Na Saladi

Vipimo
Nyama ya kusaga (Beef Regular) 2LB
Tangawizi na Thomu iliyosagwa 1 Kijiko cha soup
Chumvi kisia
Kiitunguu maji kilichosagwa (Crushed) 1 Kikubwa
Yai 1
Chenga za Mkate (bread crumbs) 1 Kikombe
Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo 1 Kikombe
Parsely iliyokatwa ndogo ndogo 1 Kikombe
Pili pili manga ya powder 2 Vijiko vya chai
Bizari ya pilau ya powder (cummin) 2 Vijiko vya chai
Mafuta (ya kunyunyizia baada ya kupanga kabab) ¼ cup
Ni bora mafuta ya zaytuun (olive oil)
Saladi ya kumwagia karibu na kababu kuwiva (tayarisha kwa kukata na kuweka kando
Vitunguu 2
Pilipili kubwa (Capsicum) 2
Nyanya 2

1. Changanya nyama na vitu vyake kisha fanya vidonge vya oval na upange katika sinia ya kupikia katika jiko la oven

2. Nyunyiza mafuta kidogo kote
3. Zipike kwa moto wa juu (broil) mpaka zipikike huku
Unazigeuza upande wa pili.
4. Karibu na kuwiva kabisa mwagia vitu ulivyotayarisha na uchanganye
na ziwache ndani ya jiko kwa dakika
5. Ziepue haraka na uziweke katika Sahani ya kupakulia nzuri zikiwa tayari kuliwa.
Unaweza kutolea na mkate au wali

Wali Wake:
Mchele Basmati (osha na kuroweka ) 3 Vikombe
Kitunguu kilichokatwa (chopped) 1 medium
Tomato iliokatwa ndogo ndogo (chopped) 1 medium
Mafuta 2 kijiko cha soup
Thom (iliyosagwa) 1 Kijiko cha Soup
Mdalasini mzima 1 kijiti
Hiliki 2 chembe
Karafuu 5 – 7 chembe
Chumvi Kisia
Bizari ya manjano (Haldi) ½ kijiko cha chai
Maji ya kupikia wali 5-6 vikombe
Stock (Maggi cubes au aina yeyote) 3 cubes
Namna Ya Kupika Wali
1. Kaanga kitunguu, kwa mafuta hayo, kabla ya kugeuka rangi tia tomato
2. Weka vitu vyote vingine isipokuwa stock ukaange kidogo.
3. Tia mchele kisha maji, stock cubes na ufunike wali upike katika moto mdogo.
4. Pakua katika sahani kisha mwagia Kabaab juu yake.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


