Choroko Za Sosi Ya Nyanya Kwa Nazi

Choroko Za Sosi Ya Nyanya Kwa Nazi
 


 

Vipimo:

 

Choroko  - 2 vikombe

Kitunguu maji  - 1 kimoja

Bizari ya manjano ya unga -   nusu kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi - vijiko 2 vya chai

Nyanya 2 - zisage 

Kitungu maji - 1 katakata 

Chumvi -  kiasi 

Tui la nazi zito - 2 vikombe viwili

mafuta - kijiko 1 cha supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Osha choroko vizuri na roweka kwa muda, kisha chemsha kwa maji ya kiasi tu hadi ziwive na zisivurugike, na zibakie supu yake kidogo tu
  2. Weka sufuria jikoni na moto wa kiasi tia mafuta kidogo.
  3. Kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi kidogo
  4. Halafu mimina nyanya iliyosagwa, kaanga hadi ziwive
  5. Tia bizari zote.
  6. Kisha mimina choroko na mimina tui la nazi
  7. Mwisho ukipenda katia pilipili ziwivie kiasi.
  8. Mimina kwenye bakuli lako tayari kwa kuliwa kwa wali, chapati n.k.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

Share