Faluda (Pakistani)

Faluda   (Pakistani)

VIPIMO:  Kutengenezea glass 12 
Tambi-  200 - 300 gms

Jelly  ya Cherry - 2 pkts ndogo

Condensed milk -  1 tin

Fruit Cocktail au peaches (cubes)(ukipenda) -  1 tin

Vanilla Ice-cream - kiasi

Rose Syrup - kiasi  

Habbat Rayhaan (Basil Seeds) -  1 tablespoon

au kwa jina la Kipakistani ni Tukhme-Rayhaan

(sio lazima ukipenda) – Rowanisha  

NAMNA YA KUTAYARISHA 

  1. Tengeneza Jelly kama inavyoeleza katika pakti. Inapokuwa tayari imeganda ikate kate vipande vya cubes.
  2. Chemsha tambi, chuja maji weka kando.
  3. Katika glass, gawa vitu vyote na kupanga kwa mpango huu:
  4. Tambi   
  5. Weka jelly cubes   
  6. Weka fruit cocktail au peaches
  7. Tia condensed milk
  8. Tia Habbat-Rayhaan kama ½  teaspoon  
  9. Tia scoop za ice-cream  mbili
  10. Mwisho tia rose Syrup kidogo juu ya ice-cream na tayari kuliwa.

 

 

Share