Uwa La Matunda

Uwa La Matunda

    

Vipimo

Nanasi - 1

Tikiti la asali la kijani (honey dew) -  1  

Shammaam (tikiti, cantelope) - 1 

Machungwa -  2 

Balungi (grape fruit)  -  ½ 

Zabibu za kijani -  3 misongo (bunches) 

Plamu (plums) -  7 – 9 kiasi 

Stroberi (strawberries) -  7 – 9 kiasi  

Namna Ya kutayarisha

  1. Kata kichwa cha nanasi, osha  kiweke katikati ya sinia ya kupakulia.
  2. Katakata matikiti yote vipande virefu virefu upange kwa mpangilio, weka kwanza tikiti la kijani kiasi, kisha weka tunda jengine kama plamu au stroberi, kisha weka vipande vya Shammaam kiasi, vipande vya nanasi uzungushe sahani hivyo hivyo.
  3. Tupia tupia matunda mengine baina ya matikiti kuleta shepu ya mauwa, na weka stroberi moja juu ya kichwa cha nanasi.  

 Kidokezo:

Unaweza kubadlisha au kuongeza matunda mengine kama tikiti maji (water-melon), peya, tufaha, peache, machenza n.k.

 

 

 

 

 

Share