Skip to main content

Kastadi Ya Biskuti

Kastadi Ya Biskuti



Vipimo

Mayai - 2



Maji - 3 Gilasi



Unga wa ngano - 3 vijiko vya supu



Nido (maziwa ya unga) - 2 gilasi



Sukari -  1/2 - 3/4 gilasi



Bisikuti za kawaida plain



Chocoleti

Vanilla - Kiasi 



Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tia maji kwanza kwenye blenda pamoja na hivyo vyote; na iache ichanganyikane vizuri.
  2. Kisha tia mchanganyiko kwenye sufuria na tumia mwiko ukoroge moto mdogo na upike mpaka ishikane kama kastadi.
  3. Kisha twaa bakuli utie nusu ya hiyo kastadi upange biskuti kati kati halafu utie nusu nyingine ya hiyo kastadi juu ya hizo biskuti na kisha kwaruzia chokoleti juu yake.
  4. Halafu weka kwenye firiji.
  5. Iache iwe baridi kisha pakuwa kwenye vibakuli na itakuwa tayari kuliwa.



Kidokezo:

Inategemea na kipimo cha gilasi kupata saizi ya kastadi.