Desert Ya Tambi Kwa Fruit Mchanganyiko Na Cream

Desert Ya Tambi Kwa Fruit Mchanganyiko Na Cream 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

 

Tambi -   200 gms takriban vikombe 2

Cream au maziwa mazito (condensed) -  1 gilasi

Maziwa ya kawaida -  2 gilasi takriban

Sukari -  ½ gilasi

Fruti mchanganyiko ya kibati - 1 kibati kikubwa

Habbat hamraa au habbat rayhaan - 2 vijiko vya kulia

(basil seeds)

Arki au vanilla - 1 kijiko cha chai

Hiliki - ½ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Roweka habbat hamraa au kwa jina jengine habbat rayhaan katika kikombe robo maji, uziache dakika chache zifure/zivimbe.
  2. Chemsha maji ya moto, yakichemka tu, tia tambi kisha haraka zitoe uzichuje. Usiache zichemke sana mpaka zikalainika sana.
  3. Mimina tambi katika bakuli kubwa.
  4. Changanya na fruit cockatail ya kibati pamoja na maji yake. Kisha changanya vitu vyote vyengine pamoja na habbat hamraa ukoroge vichanganyike vizuri. Ukiona nzito ongezea maziwa ya maji.
  5. Weka katika fridge ipate ubaridi ikiwa tayari kupakuliwa katika vibakuli.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share