Je Nitakuwa Nimeachika Ikiwa Mume Ananiingilia Kwa Njia Isiyo Ya Halali?

SWALI:

Asalamu alaykum,

Mume wangu anapenda kuniingilia kinyume na sheria, na tendo hili ameshanifanyia mara nyingi kwa nguvu, nilipoenda kwa shekhe kuulizia akaniambia tayari talaka imeshatoka kwani sheria hairuhusu tendo hilo, hivyo naomba ufafanuzi zaidi juu ya maada hiyo tafadhali.

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake, Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka siku ya Mwisho.

 

Kuingiliwa nyuma na mume ni kitendo kiovu kabisa na haimpasi mke kumuachia mumewe aendelee kufanya hivyo, bali lazima mke atafute suluhisho ima awaite jamaa zake mume na jamaa zake mke wajadaliane jambo hili haraka iwezekanavyo.

 

Pindi mume akishikilia bado kutaka kukuingilia kwa nyuma basi mke una haki kudai talaka bali inakupasa utake kuachika naye kwani ni tendo ambalo limelaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama tulivyoeleza katika Jibu lifuatalo ambalo tayari limeshaulizwa lenye maelezo kamili kuhusu hukmu ya mume kumuingilia mke kwa njia ya nyuma:

Mume Wangu Ananitaka Njia Isiyo Ya Halali

 

Kukuingilia kwa nyuma kabla haijamaanisha kwamba tayari umeshaachika kama alivyokuambia huyo Shekhe uliyemuuliza. Na hili ni jambo la hatari jengine la kuuliza watu wasio na elimu ya sheria za dini. Inapasa Muislamu aulize kwa wenye ujuzi ili apatae jibu sahihi kwani huenda ikasababisha kuvunjika ndoa wakati suluhisho linawezekana kupatikana.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share