Ndoa Ya Waliofanya Zinaa

 

SWALI:

Asalaam  Alaikum  Warahmatulhaahi  Wabarakaatuhu,  mimi  sijambo [ Al Hamdulillaah] kama  nanyi  hamjambo viongozi  wetu wa Dini  ya kweli basi ni kheri. Naomba msaada mnijibu

 Walioanza kufanya zinaa kabla ya ndoa, wakitaka kuoana wanaruhusiwa?

 



 

JIBU:

Shukrani zote anastahiki Allaah, Mola wa viumbe vyote. Pia shukrani ni kwa ndugu zetu kwa kaka na dada zetu wanaouliza maswali na kaka yetu huyu ambaye ameuliza haya maswali takriban tisa

Watu hao wawili wanaruhusiwa kuoana baada ya kukamilisha masharti Fulani. Sharti muhimu sana ni kujuta kwa kitendo hicho na kuomba msamaha kwa kufanya hivyo na azimie kutorudia tena, na lau kungekuwa na dola ya Kiislamu basi angejipeleka ili ahukumiwe, na pia kufanya mambo mazuri kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Mche Allah popote pale ulipo. Na fuatisha baya kwa zuri nalo litalifuta hilo baya” (At-Tirmidhiy kutoka kwa Mu‘aadh na Abu Dharr [Radhiya Allaaahu ‘anhu]).

Na baada ya kufanya hivyo hawatakiwi kukaa pamoja na wale wasifanye kitendo hicho mara nyingine. Wanatakiwa wawe mbali kwa muda wa miezi mitatu ili kuhakikisha kama mwanamke ana mimba au hana. Ikiwa ana mimba, mtoto huyo hatakuwa wa mwanamume huyo na wala hawawezi kurithiana. Baada ya muda huo watu hao wawili wataweza kuoana kwa kufunga ndoa na kufuata masharti ya ndoa katika Uislamu. Allah Anasema:

Mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo ya. Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke meharimishwa kwa Waumini(24: 3).

 

Tanbihi: Uislamu umefanya ndoa kuwa ni nyepesi kutekelezeka hivyo ni kwa vijana na wasichana wasijipeleke katika mambo ambayo yanaleta matamanio badala yake waoane na hili linapunguza mengi na pia kujiondoa na mengi yaliyo machafu na ya uasherati. Na Mtume ametupatia kinga pale alipowahutubia vijana:

“Enyi kongamano la vijana! Yule mwenye uwezo wa kuoa na afanye hivyo, kwani hilo linamfanya ainamishe macho yake na inahifadhi utupu wake. Ama kwa yule asiyeweza basi afunge, kwani kufanya hivyo ni kinga kwake” (Al-Bukhaariy).

 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali soma majibu yalioko katika viungo vifuatavyo:

Ndoa Ya Wazinifu

Ndoa Baada Ya Kutubu Zinaa

Wazinifu Waliotubu Wanaweza Kufanya Ndoa Na Waliotakasika?

 

Wa Allaahu A'alam

 

Share