Kamba Wa Unga Wa Dengu

Kamba Wa Unga Wa Dengu  

Vipimo

Kamba   wakubwa  - 1 pakiti

Unga wa dengu - 1 Kikombe cha chai

Pilipili ya unga - Kiasi unavyopenda

Yai - 1

Chumvi - Kiasi

Bizari ya giligilani ya unga - ¼ Kijiko cha chai

Maji - Kiasi ya kuchanganyia

Mafuta ya kukaangia           

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chambua maganda ya kamba na bakisha mikia tu.
  2. Kwenye bakuli, changanya unga, chumvi, pilipili, bizari, yai na maji kisia ili mchanganyiko usiwe mzito sana.
  3. Weka mafuta katika karai yapate moto.
  4. Chovya kamba kwenye mchanganyiko wa dengu kwa kukamata mkia na uzikaange mpaka zigeuke rangi.
  5. Weka katika karatasi au chujio zichuje mafuta na zitakuwa tayari kuliwa na chatini upendayo.

 

 

Share