Samaki Wa Samoni Mwekundu (Pink Salmon) Na Rojo La Viazi

Samaki Wa Samoni Mwekundu (Pink Salmon) Na Rojo La Viazi

  

Vipimo    

Samaki wa samoni mwekundu  (Pink Salmon) -  5- 6 vipande

Viazi - Menya, kata slaisi nyembamba za round - 2

Nyanya/tungule zilokatwa vipande vikubwa kiasi - 2

Kitunguu kilichokatwa vipande vikubwa kiasi - 1

Kitunguu saumu (thomu/galic) - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi - 1 kijiko cha supu

Ndimu - 2

Pilipilii nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Kidonge cha supu au kikolezo cha unga - 1 kijiko cha supu

Majani ya dill - kiasi

Namna Ya Kupika:   

  1. Katika kibakuli kidogo, tia maji ya moto yaliyochemka kiasi cha ¼ kikombe kisha tia kidongo cha supu au kikolezo cha unga (seasoning powder) ukoroge.  
  2. Tia, kitunguu thomu, pilipili mbichi, ya unga, chumvi, ndimu changanya vizuri.  
  3. Panga vipande vya samaki katika treya ya oveni iliyopakwa mafuta. 
  4. Paka mchanganyiko katika samaki juu na chini, bakiza mchanganyiko kidogo.  
  5. Mwagia nyanya, kitunguu, na viazi pamoja na mchanganyiko ulobakia. 
  6. Funika upike kwenye oveni, kwanza moto wa chini (bake) kisha karibu na kuiva vitu vyote, zima moto, washa moto wa juu umalizie kuivisha.    
  7. Epua akiwa tayari kuliwa na wali au mkate.  

Majani ya Dill:

 

 

 

 

 

Share