Skip navigation.
Home kabah

Kunde Mbichi Za Nazi

 

 

 

Vipimo:

 

Kunde                                                        4 Vikombe

Tui la nazi                                                   2 Vikombe

Vitunguu-maji                                             2

Kitunguu saumu(thomugalic) iliyosagwa      1 Kijiko cha supu

Pilipili mboga nyekundu                               ½                                  

Pilipili mbichi                                                2

Nyanya ya kopo                                        ½  Kijiko cha chai

Mafuta                                                      ¼ Kikombe         

Chumvi                                                    kiasi

                           

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

 

  1. Osha kunde vizuri;
  2. Chemsha kiasi cha Maji katika sufuria
  3. Mimina kunde hizo katika hayo maji yanayoendelea kuchemka na ziache zichemke hadi utakapoona zimeiva vizuri;
  4. Epua na kisha ziweke pembeni;
  5. Mimina mafuta katika sufuria hadi yachemke kisha uweka vitunguu-maji na kaanga kiasi tia thomu na endelea kukaanga hadi iwe kahawia (hudhurungi);
  6. Weka nyanya ya kopo na ikaange kwa muda kiasi katika mchanganyiko huo;
  7. Mimina kunde katika mchanganyiko huo na kisha weka Tui la nazi na acha ichemke kwa dakika kadhaa;
  8. Kisha tia chumvi kiasi na uache zichemke na kuchanganyika vizuri na kubaki rojo kiasi;
  9. Pakua tayari kuliwa.
Rudi Juu