Mchicha Wa Bamia Na Sosi Ya Nyama

Mchicha Wa Bamia Na Sosi Ya Nyama

 

 

Vipimo

 

Mchicha uliokatwa mdogomdogo - 600 gm            

Bamia (kata ndogo ndogo) -  2 Vikombe

Nyama ya ng'ombe kata vipande vidogodogo - 2 LB 

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha chai

Pilipili mbichi iliyosagwa (au nyekundu ya unga) -  1 Kijiko cha chai

Vitunguu (kata vidogovidogo) -  3     

Nyanya (kata ndogo ndogo) -  3

Nyanya ya kopo - 3 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Mafuta  -  ¼ kikombe

Chumvi  -  kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Chemsha nyama kwa maji ya kiasi, chumvi, thomu na tangawizi, pilipili, na kitunguu kimoja. Hakikisha maji    sio mengi ili itakapowiva ibakie supu yake kidogo tu.
  2. Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu mpaka viwe vyekundu kidogo, tia thomu kaanga kidogo tu.  
  3. Tia nyanya kaanga mpaka zilainike, tia nyanya ya kopo.
  4. Weka mchicha na bamia endelea kukaanga.
  5. Mimina supu ya nyama, ongeza chumvi ikibidi, iwache kwenye moto kidogo kuwivisha mchicha na bamia..
  6. Mimina katika bakuli na ikiwa tayari kuliwa.
  7.  

 

 

Share