Hukmu Ya Swawm Ikiwa Amelala Na Janaba Hadi Jua Likatoka
SWALI:
swali langu ni ikiwa mtu amelala na janaba mpaka jua likatoka jee swaum inafaa amaitakuwa haifai
shukranwa jazakum Allaah bil kher
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tumewapa nasaha mara nyingi kuwa haipasi kufanya mchezo na amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Amri za kufunga Swawm, kuitimiza ipasavyo, kwa wakati wake na ruhusa ya kufanya yote anayojizuia mja kwa wakati wake yanapaswa yote yatekelezwe bila ya kwenda kinyume au kudharau.
Swalah ya Alfajiri hata bila ya kuwa na Swawm inampasa Muislamu aitekeleze kwa wakati wake nao ni kuanzia Alfajiri hadi kabla ya jua kuchomoza. Sasa vipi Muislamu asiswali asubiri hadi jua lichomoze ndio atake kuswali? Huo utakuwa sio tena wakati wa Swalah hiyo, kwa hivyo utakuwa hukutimiza Swalah hiyo ya Alfajiri
((من نسي صلاة أو نام عنها ، فكفارتها أن يصليها إذا ذكرها، لا كفارة لها إلا ذلك)) رواه مسلم
((Atakayesahau Swalah au ikampita akiwa amelala basi kafara yake ni kuiswali atakapokumbuka, hakuna kafara isipokuwa hiyo)) [Muslim]
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


