Surat Yaasiyn, Je, Inafaa Kumsomea Mtu Anayekata Roho?

 

SWALI:

Assalam aleykum, natumaini hamjambo  kwa hiyo tunashukuru mungu anasaidia.

napenda kuuliza swali,
surat-yaasin inafaa kumsomea mtu akiwa anataka kukata roho (yaani sakarat mauti) au kama mtu amekufa kumsomea pia inafaa, au kama wewe mwenyewe unayekata roho pia inafaa,naomba jibu inshaalah mungu atakuwezesha.


 

JIBU:

Alhamdulillah,  Waswalaatu Was-salaam 'alaa Rasuli-Llah  صلى الله عليه وآله وسلم Amma ba'ad,

Tunakushukuru kwa kuuliza swali hili muhimu kuhusu Surah Yaasiyn ambayo imeenea katika mujtama'a wetu kuitumia na kuitukuza sura hii pekee kuliko surah zingine katika Qur'aan au kuitumia mahali pasipofaa.

Hadiyth inayosema, "Wasomeeni maiti wenu (wanaokata roho) Yaasiyn" ni Hadiyth dhaifu haina mashiko yoyote.

 
Hivyo, hakuna uthibitisho wa Hadiythi yoyote iliyo sahihi kuwa zimetajwa fadhila za Surah hii.  Na kwa kupata maelezo zaidi tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho upate ushahidi wa hizo Hadiyth zilizokuwa dhaifu kuhusu Surah hii.

Surat Yaasiyn Na Al-An'aam Zina Fadhila?

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

 

Share