Wazazi Wa Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Ni Watu Wa Peponi Au Motoni?
SWALI:
Ustadh nilikuwa nataka kuuliza kuhusu baba na mama yake mtume Muhammad (saw) ni watu wa motoni au wa peponi?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako
Kukatazwa huku kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwa sababu ya mama yake kutokuwa Muislam. Allaah Aliyetukuka Anatufahamisha:
“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, ijapokuwa ni jamaa zao, baada ya kwishabainika kuwa hao ni watu wa Motoni” (9: 113).
Ifahamike kuwa baba na mamake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hawakuwa Waislamu nao waliaga dunia katika ukafiri. Ama kuwa wataingia Motoni au Peponi
“Wala haikuwa Ibraahiym kumtakia msamaha baba yake ila kwa sababu ya ahadi aliyofanya naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui ya Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym alikuwa mwingi wa kuomba, mnyenyekevu, mvumilivu” (9: 114).
Nabii Ibraahim (‘Alayhis Salaam) anamuambia babake:
“Ewe baba yangu! Usimuabudu Shetani. Hakika Shetani ni mwenye kumuasi Mwingi wa Rehema” (19: 44).
Alipoona babake hasikii alijitenga naye: “Nami najitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Allaah. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi” (19: 48).
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


