Mambo Matano Uwezayo Kuwafanyia Wazazi Waliofariki Kama Kwamba Wako Hai-1
24 Muharram 1429
Wazazi wetu ndio sababu ya kuumbwa kwetu na kuweko duniani kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na kupata ridhaa zao ndio sababu ya kuingizwa kwetu Peponi
Jibu ni kwamba tunaweza kuendelea kuwatendea wema
Hadiyth ifuatayo inaanza kutaja amali tano ambazo Muislamu anaweza kuwafanyia wazazi wake waliokwisha aga dunia:
عن أبي أسيد مالك بن ربيعة رضي الله عنه قال: بينا نحن جلوس عند رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا جاءه رجل من بني سلمة فقال يا رسول الله هل بقي من بر أبوي شيء أبرهما به بعد موتهما ؟ قال: ((نعم الصلاة عليهما, والاستغفار لهما, وإنفاذ عهدهما من بعدهما, وصلة الرحم التي لا توصل إلا بهما, وإكرام صديقهما )) رواه ابن حبان في صحيحه أبو داود وابن ماجه
Kutoka kwa Abu Asyad Maalik bin Rabiy’ah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Tulipokuwa tumekaa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mtu kutoka [kabila la] Bani Salamah akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, ‘Je, kuna kilichobakia katika wema ninaoweza kuwafanyia wazazi wangu baada ya kifo chao? Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) akajibu, ((Ndio, kuwaswalia [yaani kuwaombea du’aa] kuwaombea maghfirah, kuwalipa deni [au ahadi] zao, na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao, na kuwakirimu rafiki zao)) [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, Abu Daawuud na Ibn Maajah]
1- Kuwaswalia (kuwaombea du’aa)
Ni miongoni mwa amali tatu ambazo zinaendelea kumfikia mja yeyote aliyefariki
((إذا مات إبن آدم إنقطع عمله إلا من ثلاث, صدقة جارية , أو علم ينتفع به, أو ولدٌ صالح يدعوا له)) مسلم
((Anapokufa mja hukatika amali zake zote isipokuwa mambo matatu, Sadaqah inayoendelea, au elimu yenye kunufaikiwa, au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim]
Ni amri pia kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anaposema:
(( وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا))
((Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyonilea utotoni)) [Al-Israa: 23-24]
Hii ni du’aa mojawapo ya kuwaombea
Du’aa za kuwaombea wazazi waliofariki
Katika Qur-aan:
رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا
Rabbir-Hamhumaa Kamaa Rabbayaaniy Swaghiyraa.
Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyonilea utotoni. [Al-Israa: 24]
رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَاب
Rabbana-Ghfir Liy Waliwaalidayya Walil Mu-uminiyna Yawma Yaquumul Hisaab.
Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu. [Ibraahiym: 41]
رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ
Rabbighfir Liy Waliwaalidayya
Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu. [Nuuh 28]
رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
Rabbighfir Liy Waliwaalidayya Waliman Dakhala Baytiya Mu'uminaw-Walil Mu'uminiyna Wal Mu'uminaati
Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. [Nuuh: 28]
Katika Sunnah:
Maiti mwanamume
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه، وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir lahu Warhamhu, wa'aafihi wa’afu 'anhu, wa-akrim nuzulahu, wawassi' mudkhalahu, waghsilhu bil-maai wath-thalji wal-barad, wanaqqihi minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, wa-abdilhu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wazawjan khayran min zawjihi, wa-adkhilhul jannah, wa-a’idh-hu min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar
Maana yake:
“Ewe Allaah, Msamehe na Umrehemu na Umuafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Upanue kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Peponi na Mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).
Maiti mwanamke
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُا وَارْحَمْـها، وَعافِهاِ وَاعْفُ عَنْـها، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـها، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَها، وَاغْسِلْـهُا بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِا مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُا داراً خَـيْراً مِنْ دارِها، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـها، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِها، وَأَدْخِـلْهُا الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُا مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir lahaa Warhamhaa, wa'aafihaa wa’fu 'anhaa, wa-akrim nuzulahaa, wawassi' mudkhalahaa, waghsilhaa bil-maai wath-thalji wal-barad, wanaqqiha minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, wa-abdilhaa daaran khayran min daarihaa, wa ahlan khayran min ahlihaa, wazawjan khayran min zawjihaa, wa-adkhilhal jannah, wa-a’idh-ha min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar
Kuwaombea wazazi wawili:
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُما وَارْحَمْـهما، وَعافِهِما وَاعْفُ عَنْـهما، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهما، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهما، وَاغْسِلْـهُما بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِما مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُما داراً خَـيْراً مِنْ دارِهما، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهما، وأََزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِما وَأَدْخِـلْهُما الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُما مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir lahumaa Warhamhumaa, wa'aafihimaa wa’fu 'anhumaa, wa-akrim nuzulahumaa, wawassi' mudkhalahumaa, waghsilhumaa bil-maai wath-thalji wal-barad, wanaqqihimaa minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, wa-abdilhumaa daaran khayran min daarihimaa, wa ahlan khayran min ahlihimaa, wa-azwaajan khayran min azwaajihimaa, wa-adkhilhumaal-Jannah, waa’idh-humaa min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar
Maiti zaidi ya wawili
اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُم وَارْحَمْـهم، وَعافِهِم وَاعْفُ عَنْـهم، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهم، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهم، وَاغْسِلْـهُم بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِم مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقََّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُم داراً خَـيْراً مِنْ دارِهم، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهم، وأََزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِم وَأَدْخِـلْهُم الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُم مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Allaahumma-Ghfir lahum Warhamhum, wa'aafihim wa’fu 'anhum, wa-akrim nuzulahum, wawassi' mudkhalahum, waghsilhum bil-maai wath-thalji wal-barad, wanaqqihim minal khatwaayaa kamaa yunaqqa-th-thawbul abyadhw minad-danas, wa-abdilhum daaran khayran min daarihim, wa ahlan khayran min ahlihim, wa-azwaajan khayran min azwaajihim, wa-adkhilhumul-Jannah, waa’idh-hum min ‘adhaabil qabri, wa ‘adhaabin-naar
Baadhi ya Wema Waliotangulia wametaja kwamba “Atakayewaombea wazazi wake kila siku mara tano (baada ya Swalah za fardhi) atakuwa ametimiza haki zao kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ
((Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio)) [Luqmaan: 14]
Hivyo kumshukuru Allah ni kuswali mara tano na kadhalika kuwashukuru wazazi kuwaombea kila siku mara tano” Na Allaah Anajua zaidi.
2- Kuwaombea Maghfirah:
Ni amali ya pili ambayo Muislamu anaweza kuwafanyia wazazi wake kwani kila unapowaombea maghfirah wao hupandishwa daraja Peponi:
عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ وَلَدِكَ لَكَ)) لإمام أحمد و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Peponi. Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa maghfirah na mtoto wako)) Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]
Itaendelea Insha Allaah…
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


