Mbaazi Za Mchicha Kwa Chapati

Mbaazi Za Mchicha Kwa Chapati

Vipimo: 

Mchicha uliokatwa katwa (chopped) -  400 gm    au  vikombe 3  

Mbaazi mbichi au kavu  -   *1 kikopo au  vikombe 2

Kitunguu - kimoja

Nyanya kopo - ½ kijiko cha chai

Tui la nazi zito -  1 kikombe

Chumvi - kiasi

Pilipili mbichi nzima -   2   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

*Ikiwa mbaazi sio za tayari, roweka uchemshe hadi ziwive.

Osha vizuri mchicha kisha, katakata  mdogo mdogo (chopped) au tumia ulio tayari wa barafu (frozen chopped spinach) 

Katika sufuria, tia mchicha pamoja na mbaazi zilizokwisha iva.  

Katakata kitunguu, utie humo, tia nyanya kopo, tia chumvi na pilipili mbichi nzima .

Tia tui upike katika moto mdogo mdogo hadi zitokote na kuiva mchicha, usiache zikauke sana.  Tayari kuliwa na mkate au wali. 

 Upishi wa Chapati unapatikana katika viungo vifuatavyo:

Chapati - 1

Chapati -2

 

 

Share