Nyanya Za Mshumuaa/Chungu/Ngogwe Za Nazi

Nyanya Za Mshumuaa/Chungu/Ngogwe Za Nazi

Vipimo 

Nyanya chungu - 20-25

Tui la nazi - 1 ½  kikombe

Kitunguu maji -  ½

Tungule (Nyanya)  - 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu

Bizari -  ¼ kijiko

Chumvi -  kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

1. Kosha nyanya chungu kisha zimenye uzipasue kati kati kwa urefu, itasaidia kuona kama hakuna wadudu

    ndani. 

2. Kata kitunguu maji vipande vidogo vidogo, menya tungule maganda ukate pia.  

3. Kwenye sufuria changanya vitu vyote , weka jikoni upike. 

4. Ikikaribia tui kukauka epua.  

5. Pakua kwa kijiko moja moja ili zisivurugike weka kwenye sahani tayari kuliwa.

 

Share